Nguvu za Sifa na Maombi

Nguvu za Sifa na Maombi

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; nyuani mwake kwa kusifu; mshukuruni, lihimidini jina lake! ZABURI 100:4

Silaha za kiroho ambazo Mungu hutupatia kutumia katika maisha yetu ni baraka za ajabu ambazo tunaweza kushukuru kwazo. Silaha moja muhimu tuliyo nayo ni sifa.

Sifa humshinda shetani, lakini lazima iwe sifa ya kweli inayotoka moyoni, sio tu huduma ya mdomo au mbinu inayojaribiwa ili kutambua iwapo inafanya kazi. Sifa na aina zingine zote za maombi huhusisha Neno. Tunamsifu Mungu kulingana na Neno lake na wema wake.

Maombi huzalika kutokana na uhusiano na Mungu. Ni kuja kuomba usaidizi, na kila mara kukumbuka kumsifu kwa sababu ya wema wake wote. Ni kuongea na Mungu kuhusu kitu kinachotusumbua. Ni ushirika, urafiki, na nafasi ya kuonyesha shukrani kwa jinsi yote Mungu alivyo na anayotenda. Ukitaka kuwa na maisha ya mafaniko ya maombi, kuwa na uhusiano mzuri na Bwana. Amini kuwa anakupenda, kwamba ni mwingi wa rehema, na kwamba atakusaidia ukimwomba.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa nguvu za sifa na maombi katika maisha yangu. Ninataka kuishi kila siku kwa mshangao wa yote ambayo umenitendea. Nisaidie kujumlisha sifa na maombi katika safari yangu ya kila siku na wewe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon