Nia ya Shukrani

Nia ya Shukrani

Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano. WAFILIPI 2:14

Sisi wote tunaweza kulalamila kila mara. Lakini kulalamika hakusaidii; kile ambacho kulalamika hufanya ni kufungua mlango kwa adui. Hakusuluhishi matatizo; hutayarisha tu eneo la kuzalisha matatizo makubwa zaidi.

Badala ya kulalamika, hebu tuchague kwenda mbele ya Bwana kila siku kwa nia ya shukrani. Sio tu kumshukuru mara mojamoja lakini kuendelea kuzoea kumshukuru kila siku kama desturi ya maisha yetu. Mtu ambaye ana “nia ya shukrani” ni yule mwenye shukrani na aliyejaa shukrani kwa kila kitu ambacho Mungu anafanya katika maisha yake siku baada ya nyingine.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa jinsi unavyonikimu katika kila eneo la maisha yangu. Badala ya kulalamika kuhusu kile ninachotaka au kuhusu nisichokuwa nacho, ninachagua kushukuru kwa kila kitu nilicho nacho. Umekuwa mwema kwangu—asante kwa wema wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon