Nidhamu na Kiasi

Nidhamu na Kiasi

Asiyetawala roho yake ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta. MITHALI 25:28 BIBLIA

Tunaweza kuishi maisha ya nidhamu yaliyojaa kiasi. Ni mojawapo ya funguo za maisha yaliyojaa furaha. Mahali kwingi ndani ya Biblia, tunafundishwa umuhimu wa kuishi maisha yenye kiasi.
Tusipojiadhibu, hatimaye mambo ambayo tunapitia yatakuwa hali tunazojutia, Neno la Mungu linatufundisha kuwa wenye kiasi, kutokiuka mipaka (kupata mwafaka kati ya mawazo yasiyo na kadiri au kuafikiana).

Tudumishe kiasi bila kizuizi. Eneo la fedha ni mfano wa mahali ambapo kiasi kinahitajika. Ni makosa kutumia pesa kupindukia, lakini pia ni makosa kutumia pesa kidogo. Mungu hutupatia pesa kufurahia wala sio kuweka. Hekima ina maana ya kuweka baadhi yake kama akiba, kutumia zingine na kutoa zingine.

Katika kila eneo la maisha yako—mahusiano, pesa, mazoezi, kula, kazi, fikra, na maneno—muombe Mungu ili akusaidie kuishi kwa nidhamu na kiasi. Usiongozwe na hisia unapowaza. Tumia hekima ya Mungu ili kuishi maisha ya kiasi na kwa kweli kuyafurahia!


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba umenipa tunda la kiasi, na kwa neema zako, ninaweza kujiadhibu. Unanipa nguvu na hekima, na unaniongoza katika kila hatua njiani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon