Omba kabla hujachelewa Sana

Alipofika mahali pale aliwaambia, ombeni kwamba msiingie majaribuni (LUKA 22:40)

Wanafunzi walikuwa wanajaribiwa katika njia nyingi walipokuwa wanangoja na Yesu katika Bustani la Gethsemani. Huenda walitaka kukimbia, kujificha, au kufanya vile Petro alifanya alipokana kumjua Kristo. Yesu hakuwaambia kuomba kwamba wasijaribiwe, lakini aliwaambia waombe kwamba hawataingia katika majaribu.

Lingekuwa jambo la kupendeza tusingehisi kufanya vitu vibaya, lakini halitawahi kufanyika. Biblia inasema, lazima majaribu yaje. Sababu moja ya kuwa na imani ndani ya Mungu ni ili tukatae majaribu  ya kufanya vitu vibaya. Yesu alitaka waombe mapema ndipo shinikizo likiwa baya sana, watakuwa tayari wameimarika kiasi cha kuyapinga.

Mtu akiwa na shida ya kujaribiwa na jambo fulani, ni vyema sana kuomba nguvu za kukataa kufanya uteuzi mbaya kabla haujaufanya. Kwa nini ungoje kukabiliana na shinikizo la kufanya uteuzi wa mambo mengi mazuri yanayokujaribu. Kwa kweli ninaamini kwamba, iwapo tutatambua maeneo yetu ya udhaifu na kuomba kupata nguvu kila wakati tutaona ushindi mwingi. Ninajua kwamba huwa najaribiwa kuonyesha kukosa subira ikiwa ninangoja kwa muda mrefu, kwa hivyo huwa ninaomba hata kabla ya kuingia katika hali hizo na huwa inasaidia. Mungu ametuahidi nguvu zake, lakini lazima tumwitishe.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unayaweza mambo yote katika yeye akutiaye nguvu.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon