Sema “Ndiyo” kwa Kilicho Muhimu Sana

Sema “Ndiyo” kwa Kilicho Muhimu Sana

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. MATHAYO 6:33

Ukitaka kuishi maisha yasiyo magumu sana, huenda ukahitajika kuyarahisisha kwa kutofanya mambo mengi. Watu wengi wanaokuwa na msongo wa mawazo na kufadhaika wamepungukiwa na nguvu kwa sababu wamejaribu kusukumiza mambo mengi katika ratiba zao.

Kwa hivyo jifunze kusema “la” kwa vitu vichache. Jizoeshe kuisema: “La!” ni neno rahisi ambalo huwa rahisi kusema unapozidi kulitumia. Na ujifunze kusema “ndiyo” kwa kile ambacho ni muhimu tu maishani—vitu ambavyo unaamini kwa kweli kwamba ndivyo mapenzi ya Mungu juu yako.

Tenga muda wa kuketi na familia yako na marafiki. Burudika na Mungu. Usiwe mwenye shughuli nyingi sana ukakosa kufurahia vyote ambavyo Mungu amekupa. Tenga muda wa kucheka na kushukuru kwa sababu ya uhai.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa vitu ambavyo kwa kweli ni vya muhimu katika maisha yangu. Leo ninachagua kuvifikiri vitu hivyo na kuvisahau vitu vingine vilivyo vizuizi. Asante kwa sababu, kwa usaidizi wako, ninaweza kufurahia maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon