Shukrani Tele na Kufurahia Leo

Shukrani Tele na Kufurahia Leo

Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, tutashangilia na kuifurahia ZABURI 118:24

Mara nyingi wazazi wachanga huchelewesha kufurahia mtoto wao hadi anapofika hatua fulani ya kukua kwake. Akiwa mchanga wanasema, “Nitafurahi akiacha kutumia nepi (au akiacha kung’oa meno au kuanza kutembea).” Halafu wanasema, “Nitafurahi akifika chekechea.” Kisha inakuwa, “Nitafurahi akiwa shule mchana kutwa.” Baadaye wanasema, “Nitafurahi akifuzu.”

Inaendelea hivyo hivyo hadi mtoto anakuwa mkubwa na kwenda, na kwa kweli hao wazazi hawajawahi kufurahia hatua yoyote ya maisha yake. Walikuwa wakingoja tu kila mara kufurahi siku ile. Acha nikuhimize: usiahirishe kufurahia hadi kila kitu kitimilike—shukuru Mungu kwa kila hatua njiani. Jifunze kufurahia na kufurahi ndani ya Bwana, siku hii na kila siku katika safari yako maishani.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa hatua ya maisha niliyomo sasa hivi. Hata kama ninapitia katika changamoto na matatizo, nisaidie kukumbuka kwamba umekuwa mwema kwangu, na unisaidie kuwa mwenye shukrani kwa ajili ya leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon