Siibatili neema ya Mungu; maana ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, bali Kristo alikufa bure… —WAGALATIA 2:21
Ninajua vile mfadhaiko ulivyo kwa sababu niliishi miaka mingi kwa maisha ya kufadhaika. Nilijua Mungu vile Mungu alivyokuwa, lakini nilijua machache kuhusu neema yake na jinsi ya kukaa katika uhusiano wa karibu naye. Kutokea hapo nimejifunza kwamba, ninapofadhaika, ni kwa sababu ya kwamba ninajaribu kufanya jambo lifanyike katika nguvu zangu badala ya kumngoja Mungu afanye lifanyike. Nikifadhaika ni ishara kwamba ninajishughulikia mwenyewe badala ya kumtegemea na kupokea neema yake.
Je, umefadhaika katika uhusiano wako? Katika kazi yako? Katika kutembea kwako na Bwana? Je, unang’ang’ana na eneo fulani la nafsi yako ambalo linakusababishia matatizo, au kuna mazoea fulani ya kitabia ambayo huwezi kuvunja?
Mfadhaiko huja kwa kujaribu kufanya kitu ambacho huwezi kufanya mwenyewe. Mungu pekee ndiye anayeweza kufanya mambo yafanyike katika maisha yako. Utafadhaika ukijaribu kufanya mambo bila yeye. Lakini dakika ambayo utasema, “Bwana, siwezi kufanya haya mwenyewe, kwa hivyo ninakupa wewe. Ninahiari kufanya chochote unachoniambia nifanye, lakini nitahitaji neema yao (uweza) ili nikifanye.”—ukiomba ombi hilo kwa uaminifu, utaanza kufurahia utulivu wa Bwana.
Achilia na umtumainie Mungu kukufanyia yale ambayo yeye pekee anaweza kufanya. Acha Mungu awe Mungu katika maisha yako.