Unapendwa

Unapendwa

Nasi tumelifahamu [kulielewa, kulitambua, kulijua kwa kutazama na kwa tajriba] pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi na kuliamini [kulizingatia na kutia imani ndani ya na kutegemea] upendo wa Mungu. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. —1 YOHANA 4:16

Tumeumbwa na Mungu kwa ajili ya upendo. Kupenda na kupendwa ndiyo yanayoleta thamani katika kuishi maisha. Huyapa maisha kusudi na maana. Lakini iwapo tutaruhusu dhambi na kutosamehe na yaliyopita kututenga na upendo wa Mungu itatuacha tukiwa na njaa ya upendo na huzuni.

Watu wengi hawawezi kudumisha mahusiano mazuri, kwa sababu labda hawajui jinsi ya kupokea upendo au wanadai kupewa na wengine, vitu ambavyo Mungu peke yake anaweza kuwapa. Masikitiko yanayotokea mara nyingi husababisha uharibifu wa ndoa na msongo wa urafiki.

Biblia inatufundisha kwamba Mungu hupenda kikamilifu tena bila masharti. Upendo wake mtimilifu juu yetu hautegemei ukamilifu wetu. Mungu anatupenda kwa sababu anataka kutupenda! Mungu ni upendo (1 Yohana 4:8). Upendo ndio alio. Mungu hutupenda kila mara; unachopaswa kufanya ni kupokea upendo huo na kuishi kwa tumaini kila siku tukijua kwamba upendo wake huyapa maisha yetu kusudi na maana.

Ufunuo wa upendo mkamilifu wa Mungu juu yako unaweza kubadilisha maisha yako na kutembea kwako na Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon