Unapohisi Kukata Tamaa

Unapohisi Kukata Tamaa

Mfurahieni Bwana; shangilieni, enyi wenye haki pigeni vigelegele vya furaha; ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo! —ZABURI 32:11

Watu kutoka pembe zote za maisha hushikwa ghafla na mtamauko na kupoteza matumaini. Kuna sababu nyingi za kimsingi za kupoteza matumaini na matibabu tofauti yaliyotolewa ili kukabiliana na hali hiyo. Mengi ni ya mafanikio lakini mengine hutoa tu suluhu ya muda. Habari njema ni kwamba Yesu anaweza kutuponya na kutukomboa kutokana na mtamauko. Anaweza kurejesha maisha yetu kuwa yale ya furaha na amani.

Iwapo wewe ni amwaminiye Yesu Kristo, tayari furaha ya Bwana iko ndani yako. Hata kama huonekani kuhisi furaha, unaweza kuichochea imani hiyo na kuiachilia kwa imani. Unaweza kuwa na kilicho chako kama matokeo ya imani yako ndani ya Yesu Kristo. Ni mapenzi ya Mungu kwako kuwa na furaha!

Mimi mwenyewe nilikuwa na matatizo na mtamauko na kukosa matumaini kitambo sana. Lakini shukuru Mungu nilijifunza kwamba, sikuwa na lazima ya kuacha fikra mbaya zinitawale. Nilijifunza kuachilia furaha ya Bwana katika maisha yangu! Mtamauko unapokuja, usiukubali wala kukubaliana nao, lakini jitie moyo kwa kutazama ahadi za Mungu na kuziachilia zikujaze tumaini. Haijalishi ulichopitia maishani au unachopitia sasa, kutamauka hakutabadilisha mambo. Haijalishi ulichopoteza, bado una mengi yaliyobakishwa. Acha kuishi katika siku zilizopita na umwombe Mungu akuonyeshe mustakabali aliokupangia!


Unapojaribiwa kutamauka, sema “la” kwa majaribu hayo na uwe na fikra nzuri, ukitarajia kitu chema kifanyike kwako!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon