Unapohisi Woga

Unapohisi Woga

Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. —ISAYA 41:10

Mojawapo ya faida zilizopo kwa ajili yetu kama waaminio ni uhuru kutokana na woga. Iwapo woga umekuwa na nguvu juu yako katika siku zilizopita, unaweza kuwa huru kutokana nao. Kwa usaidizi wa Mungu, unaweza kujifunza jinsi ya kushinda woga na kuwa na maisha tele tele ambayo Mungu amekupangia.

Hata kama tunahisi woga, hatuna lazima ya kukubali hisia hiyo. Tunaweza kuendelea kushughulikia kile Mungu ametuita tufanye kwa sababu Mungu atakuwa nasi kutulinda na kutufanikisha. Atatusaidia, atatutangulia kupigana vita hivyo kwa niaba yetu, na kuhakikisha kwamba tunashinda tunapozidi kumtii.

Ujumbe wa “usigope kwa kuwa niko nawe” umesemwa katika Biblia nzima. Mungu hataki tuogope, kwa sababu woga hutuzuia kusonga mbele na kufanya yote aliyotupangia kufanya. Anatupenda na anataka kutubariki, lakini woga hujaribu kutuzuia kufurahia mema ya Mungu.

Nia nzuri kabisa ambayo Mkristo anaweza kuwa nayo kwa woga ni hii: “Woga hautoki kwa Mungu, na sitauacha udhibiti maisha yangu! Nitakabiliana na woga. Sitakubali woga. Nikihisi kuogopa, nitaendelea kusonga mbele kwa sababu ninajua Mungu yuko nami.”


Yesu ni mkombozi wako. Unapomkaribia, atakukomboa kutokana na woga.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon