Upanga wa Roho

Upanga wa Roho

Tena ipokeeni chapeo ya wokovu na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. —WAEFESO 6:17

Mashambulizi ya shetani dhidi ya kanisa yamekuwa makali kushinda siku zilizopita. Watu wengi wanapitia mashambulizi makubwa dhidi ya fikra zao na kuvumilia mashambulizi makuu ya hofu.

Mtu anayejifunza kukaa ndani ya Neno la Mungu na kuruhusu Neno kukaa ndani yake atakuwa na upanga ukatao kuwili ambao atafanyia vita. Kukaa inamaanisha kubaki, kuendelea ndani ya, au kuishi ndani. Ukifanya Neno la Mungu kuwa sehemu ndogo ya maisha yako, utajua tu ukweli kwa kipimo na kuwa na uhuru ulio na mipaka. Lakini wanaoishi ndani yake watajua ukweli kamili na watakuwa na uhuru mkamilifu.

Maisha yalikuwa yamevurugika kwa sababu nilipuuza Neno. Kwa muda wa miaka mingi nilikuwa Mkristo aliyempenda Mungu na nilishughulika na kazi kanisani, lakini sikuwa na ushindi wowote kwa sababu sikulijua Neno. Ninashukuru, sasa ninaweza kushuhudia kwamba Neno la Mungu limenifanya kuwa mshindi na kutambua mashambulizi ya shetani.

Jifunze Neno na uruhusu Roho Mtakatifu alitawale kwa kulisema, kuimba, au kutafakari kuhusu vifungu vya Maandiko unavyofikiri kuwa anaweka moyoni mwako.


Ukiinua upanga wako, adui hatakuwa mwepesi wa kukukabili. Sema Neno!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon