Upendo hauna Husuda au Wivu

Upendo hauna Husuda au Wivu

. . . Upendo hauhusudu, upendo hautakabari, haujivuni. —1 WAKORINTHO 13:4

Biblia inatuambia kwamba upendo hauna husuda au wivu, lakini wivu ni kitu kidogo ambacho kinaweza kuingia katika maisha yetu kwa urahisi tusipokuwa waangalifu. Nimegundua njia nzuri ya kushinda husuda au wivu ni kukubali kwamba unao. Utakapoanza kuhisi wivu, kuwa mwaminifu kwa Mungu na umwombe akusaidie kuishi huru kutokana nao.

Nitaka kukubali kwamba, kama watu wengi, nimekabiliana na wivu wakati mwingine maishani mwangu. Kuna siku nilizosikia kuhusu baraka ambayo mtu alikuwa amepokea na nikafikiri, hilo litafanyika lini kwangu? Lakini nimejifunza kwamba mawazo kama hayo yakiingia akilini mwangu, ninahitaji kufungua kinywa changu mara moja na kusema, “Nina furaha kwa sababu ya mtu huyo, na ninakataa kuwa na husuda au wivu.”

Alama ya ukomavu wa kiroho—ya kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu—ni kuchagua kuwabariki wengine na kutokuwa na kutoogopa kwamba watatushinda. Tunaweza kuchagua kutoionea wivu sura ya mtu, mali, elimu, hadhi ya kijamii, hadhi ya ndoa, vipawa na talanta, kazi au chochote kile kwa sababu itazuia tu baraka zetu sisi wenyewe.


Kuwa na ujasiri wa vipawa na talanta ulizo nazo. Mungu amekupa kila kitu unachohitaji ili kutimiza mwito wake juu ya maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon