Upendo Katika Vitendo

Upendo Katika Vitendo

Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. —Yohana 13:35

Kama wakristo, tumeitwa kuwaonyesha wengine upendo.Kama vile maandiko yanasema, ulimwengu utajua kwamba sisi ni wafuasi wa Yesu mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. (Yohana 13:35)

Watu wengi huenda upendo kana kwamba ni hisia tu, lakini ni zaidi ya hisia tu. Upendo halisi hudhihirika katika matendo.

Matendo haya hayapaswi kuwa magumu nay a kutuchosa. Njia moja ya kuonyesha upendo wa Kristo ni kupitia njia rahisi ajabu.

Kwa mfano, kumpa mtu zawadi kidogo, au kupata muda wa kuongea na mtu aliyeshushwa moyo.

Au kumpatia kapu la chakula kwa mama asiye na mume anayengángána kuwapa wanawe chakula.

Kuonyesha upendo kwaweza kuwa harisi kama kumpa tabasamu mtu unayempita njiani, kwenye maduka au chumba cha mkutano.

Kuna njia nyingi za kuuonyesha upendo wa Kristo. Unapomuonyesha mtu yeyote yule upendo wa Kristo, kunawezesha kuufanya moyo wake mwepesi, na kwa muda kidogo, naye pia ataanza kutafuta nafasi za kuwaonyesha wengine upendo.

Kwa hivyo sherehekea upendo huu na umuache Mungu akuongoze. Je, anakunenea kumhusu mtu yeyote leo?

Ningependa upendo wangu kwa Yesu udhihirike katika namna ninayoonyesha wengine upendo – hata wale walio wagumu wa kupendwa. Ikiwa nitaweza kuufanya moyo mgumu mwepesi kupitia upendo wa Mungu, huenda moyo huo pia ukaifanya mioyo mingine miepesi, na upendo wa Mungu utazidi na kuzidi. Na baada ya muda tutakuwa na mapinduzi ya upendo.


Ombi La Kuanza Siku

Mungu, ningependa upendo wako udhihirike wazi katika namna ninayoonyesha wegine upendo. Nionyeshe njia za kuweza kuonyesha upendo huo kwa yeyote na kwa kila mtu utayenikutanisha naye.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon