Urahisi na Maamuzi

Urahisi na Maamuzi

Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape wala kwa mbingu wala kwa nchi, wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu. YAKOBO 5:12

Kufanya maamuzi kunaweza kuwa rahisi tukikataa kuwa na nia mbili. Baada ya kufanya uamuzi na tusimame imara, acha “ndiyo” yako iwe “ndiyo” na “la” yako iwe “la.” Kutofanya uamuzi na kuwa na nia mbili havileti tu kuchanganyikiwa na utata, lakini vile Yakobo alivyosema, husababisha pia hukumu (tazama Yakobo).

Tukiamua katika mioyo yetu kwamba tunafaa kufanya kitu kisha tuachilie akili zetu kutushawishi kutokifanya, tutafungua mlango wa hukumu. Mara nyingi huwa tuna wakati mgumu kufanya uamuzi na kwa kweli huku tukiwa tunahitajika tu kuamua. Omba Mungu akupe hekima na mwongozo, halafu ufanye uamuzi bila kuwa na wasiwasi kuuhusu. Shukuru kwamba huhitaji kuishi na hofu ya kukosea. Iwapo moyo wako uko sawa na ufanye uamuzi ambao haulingani na mapenzi ya Mungu na uishie kuondoka kwenye njia. Atakusamehe, akutafute na kukuregesha kwa njia.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kuepuka kutatiza mchakato wa kufanya uamuzi. Ninakushukuru kwamba unaona moyo wangu na utarekebisha njia yangu nikichukua hatua isiyofaa. Ninakushukuru kwamba ninaweza kufuata tu kile ninachoamini kwamba unaniongoza kukifanya na kukuamini kwamba utanilinda katika mchakato huo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon