Utulivu Kwa Wachovu

Utulivu kwa Wachovu

Au hamjui ya kuwa, mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa [kama zawadi]na Mungu? —1 Wakorintho 6:19

Ufunguo wa kwanza wa kushinda mfadhaiko ni kutambua au kukubali kuwa tunayo, na kutafuta chanzo chake. Kuna wakati katika maisha yangu ambapo nilikuwa nikiwa na maumivu ya mara kwa mara ya kichwa, mgongo, tumbo, shingo, na dalili zingine zote za mfadhaiko, lakini ikawa vigumu kwangu kukubali nilikuwa niking’ang’ana sana kimwili, kiakili, kihisia na kiroho. Nilitaka kufanya vitu vyote nilivyokuwa nikifanya na sikuwa nikitaka kumwuliza Mungu alichotaka nifanye. Nilikuwa naogopa atanifanya niache kitu ambacho sikuwa tayari kuacha bado.

Ingawa Bwana huwapa nguvu waliozimia na wanyonge, iwapo umechoka kutokana na kutumia mwili wako hadi ukazidi uwezo wake wa kutumika, utapata mfadhaiko. Miili yetu ni hekalu (makao) ya Mungu, na huwa tunaghairi tunapojisukumiza kupita mipaka ya kusudi la Mungu na kuishi katika mfadhaiko usiokoma. Sisi sote tuna kiasi na tunahitaji kukitambua na kuondoa mfadhaiko wa ziada kutoka kwa maisha yetu.

Ukiuchosha mwili wako, huwezi kwenda dukani na kununua mwingine, kwa hivyo tunza ulio nao!


Kupumzika mara kwa mara ni kitu cha busara unachoweza kufanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon