Ombeni bila kukoma. —1 WATHESALONIKE 5:17
Kadri tunavyomkaribia Mungu katika uhusiano naye, ndivyo tunavyokuwa na hakika katika maombi. Ukweli ni kwamba Mungu anataka tuwe na hakika na utulivu katika maombi kiasi kwamba itakuwa kama kupumua, kitendo tusichotumia nguvu kufanya na kukifanya kila dakika tuliyo hai. Hatufanya kazi na kung’ang’ana ili tupumue, na hatutaweza kufanya hivyo katika maombi iwapo tutaelewa urahisi wake.
Ili kuomba bila kukoma vile Paulo anavyosema katika 1 Wathesalonike 5:17 haimaniishi kwamba tunafaa kuwa tunatoa aina fulani ya maombi ya kiutaratibu kila dakika masaa ishirini na manne kila siku. Inamaanisha kwamba tunaweza kuwa katika hali ya maombi mchana wote. Tunakutana na kila hali au mambo yanayohitaji kushughulikiwa yanapokuja katika mawazo yetu, tunawezesha kuyasalimisha kwa Mungu kupitia kwa maombi. Huwa nasema kila mara “Ombea njia zako mchana wote.”
Usisahau: Sio urefu, sauti au ufasaha ambao hufanya yawe na nguvu—maombi hufanikishwa kwa uaminifu na imani inayoambatana nayo.
Tunaweza kuomba tukiwa mahali popote wakati wowote kuhusu chochote. Maombi yetu yanaweza kuwa ya sauti au ya kimoyomoyo, marefu au mafupi, hadharani au faraghani—la muhimu ni kwamba tunaomba.