Watendaji wa Neno

Watendaji wa Neno

Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. —YAKOBO 1:22

Sehemu muhimu ya kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu ni kujifunza kuwa watendaji wa Neno wala sio wasikiaji tu. Tukisoma na kusikia Neno, lakini tupuuze kufuata maagizo linalotupatia, tutaishi kwa kupungukiwa na mema ya Mungu juu ya maisha yetu.

Ni ukweli wa Neno la Mungu—na huo ukweli peke yake—ndio utatuweka huru. Ili ukweli huo ufanye kazi ndani ya maisha yetu, ni muhimu kuutenda. Utiifu kwa Neno lake ndio huleta amani, furaha, na maisha ambayo yamebarikiwa kwa njia nyingi.

La muhimu ni hili: Mungu ni Msaidizi wako. Ni Mponyaji wako. Ana mpango maalum kwa ajili yako katika Neno lake. Kadri unavyosoma, kujifunza na kutii Neno lake, ndivyo unavyojifunza jinsi mpango huo ulivyo na kuanza kuutimiza kutoka kwa hatua moja hadi nyingine. Kutii Neno huhitaji uamuzi thabiti—ni mchakato wa kila siku. Kadri unavyojifunza Neno la Mungu zaidi ndivyo unavyojifunza kulipenda. Kitu cha ajabu hufanyika unapogundua maagizo na ahadi za Mungu zinazopatikana katika Neno lake. Utataka kurudia lingine zaidi kila wakati!


Utatembea katika ushindi ukifanya uamuzi kufanya vile Mungu amesema.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon