Wewe Ni Mahali Pa Maombi

Wewe ni Mahali pa Maombi

Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu. —1 Wakorintho 3:9

Chini ya Agano la kale, hekalu ilikuwa makao ya Mungu, mahali pa maombi pa watu wake, wana wa Israeli. Hekalu ilikuwa na sehemu tatu, moja ilikuwa mahali patakatifu ndani ya pazia, na ilibeba uwepo wa Mungu! Ajabu kwamba sasa roho zetu zilizogeuzwa na kusafishwa ndizo mahali ambapo uwepo wake huishi!

Chini ya Agano Jipya, Mtume Paulo anatuambia kuwa uwepo wa Mungu sasa ni siri tuliyojulishwa, kwamba Kristo ndani yetu “Tumaini la utukufu” (Wakolosai 1:27). Kwa sababu ya umoja ulio nao sasa pamoja na Kristo, unaweza kuwa karibu na Mungu kwa sababu wewe ni hekalu hai ya Mungu. Roho Mtakatifu anaishi ndani yako, jengo linalojengwa bado, na makao yake pia, hema lake. Paulo anazidi kutuhimiza tuishi maisha matakatifu kwa kuwa sisi ni hekalu ya Mungu.

Wana wa Israeli walikuwa wakienda mahali maalum kutwaa ibada zao kwa maagizo ya kina, sisi tuna faida ya ajabu ya kumwabudu Mungu mahali popote, kwa wakati wowote. Kwa hivyo tunaweza kuitwa nyumba ya maombi.


Tuko karibu na Mungu kila wakati kwa sababu anaishi ndani yetu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon