Wewe ni Mjumbe wa Kristo

Wewe ni Mjumbe wa Kristo

Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anaishi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. WAKORINTHO 5:20

Mungu wakati wote huwa anawaambia watu wake na bado anatuambia: “Mimi na wewe ni washirika. Wewe ni mwili wangu ulimwenguni leo.” Sisi ndivyo viwakilishi vya jinsi Mungu alivyo. Sisi ni mdomo wake, mikono yake, miguu yake, uso wake. Sisi ndio huonyesha vile roho yake ilivyo, kuonyesha upendo wake na kuwafunulia walio karibu nasi uwezo wake. Jamani ni faida ilioje ya kushukuru kwayo!

Tunafaa kuvutiwa kuomba kwa unyenyekevu kila siku, “Baba, asante kwa kuwa nina nafasi ya kuwa mwakilishi wako duniani leo. Asante kwa kunitumia.” Tutakuwa na hekima pia kuomba ili tupate hekima na rasil-mali za mbinguni kwa ajili yetu na wenzetu. Kwa neema ya Mungu, tunaweza kushirikiana naye ili makusudio yake yatimie katika maisha yetu na katika maisha ya wale walio karibu nasi.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba unamwaga hazina yako katika vyombo vya udongo. Asante kwamba unanitumia kuonyesha upendo wako, huruma, uwezo na neema kwa ulimwengu unaonizunguka. Nisaidie kuwa mjumbe wako kwa dunia leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon