Acha “Mwamuzi” Atoe Wito

Acha “Mwamuzi” Atoe Wito

Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. —WAKOLOSAI 3:15

Katika Wakolosai 3:15, Paulo anatuambia kwamba amani ni kama mwamuzi—inatoa mwito katika maisha yetu, kutoa suluhu kwa kila jambo linalohitaji kufanyiwa uamuzi.

Hilo linamaanisha tu kwamba usipokuwa na amani kuhusu uamuzi au kitendo, usiendelee nacho. Acha “mwamuzi” atoe wito. Baadhi ya watu hufanya uamuzi wa kazi ambayo kusema ukweli hawakuwa na amani nayo, halafu wanashangaa ni kwa nini wana mfadhaiko na hawana furaha katika kazi zao. Watu wengi hununua vitu vingi vya bei ghali hata kama hawana amani kuvihusu, kisha wanaendelea kupoteza amani yao kila mwezi wanapofanya malipo ya vitu hivyo.

Lakini tunaweza kuacha amani ya Kristo “itawale (iwe kama mwamuzi mfululizo)” katika mioyo yetu. Kuwepo kwa amani kutatusaidia kufanya uamuzi kuhusu masuala yanayoibuka akilini mwetu kwa uhakika. Unapochukua muda katika maombi na Neno la Mungu kila mara, utatambua hekima na maarifa makuu kutoka kwa Bwana. Hutakuwa na haja ya kufikiri nifanye au nisifanye? Hili ni jambo ninalofaa kufanya au ni makosa? Kama mwana wa Mungu, ambaye anaishi katika uhusiano wa karibu na Baba yake wa mbinguni, utaweza kufuata amani anayokupa.


Unapokosa kuwa na uhakika wa kile utakachofanya, fuata amani kila mara!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon