Furaha ya Kuamini

Furaha ya Kuamini

Pasipo maono, watu huacha kujizuia… —MITHALI 29:18

Kitabu cha Mithali kinasema kwamba pasipo maono, watu huacha kujizuia. Maono ni kitu tunachoona katika akili zetu, “kuona kiakili” vile linavyofafanuliwa kwingine. Huenda kikawa kitu ambacho Mungu ameweka mioyoni mwetu au kitu tunachotaka kuona kikifanyika na tumekikabidhi kwa Mungu kwa maombi. Maono juu ya maisha yetu huhusisha vile tunavyofikiria kujihusu pamoja na mstakabali wetu.

Nimegundua kuwa baadhi ya watu wanaogopa kuamini watapata kitu kizuri. Wao hufikiria huenda wanajitayarisha kwa masikitiko. Hawajawahi kukugundua kuwa wataendelea kusikitika iwapo hawataamini.

Ninahisi kwamba iwapo nitaamini kwa ajili ya kupata vingi na nipate nusu yavyo, niko afadhali kuliko kukosa kuamini kwa ajili ya kitu na kukosa vyote. Ninataka kukuhimiza kuanza kuamini kwa ajili ya vitu vizuri. Amini unaweza kufanya unachohitaji kufanya maishani kupitia kwa Kristo. Ukiamini, inachochea imani katika moyo wako, na imani humpendeza Mungu, na kukuleta karibu naye.

Jiepushe kuwa na nia ya roho ya “haitawahi kufanyika.” Achilia imani yako kupaa. Iwapo hauna hakika vile utakavyofanya hivyo, anza kwa kuchukua orodha ya mawazo yako. Umekuwa ukiwaza na kuamini nini hivi karibuni? Jibu la ukweli litakusaidia kuelewa sababu ya kutopokea kile umekuwa ukitaka kupata.


Mungu ametualika kuomba kwa ujasiri, kwa kutumainia wema wake juu yetu, na ninapendekeza uanze leo!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon