Kufikiria Wengine Kwanza

Kufikiria Wengine Kwanza

Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. —WARUMI 12:3

Unyenyekevu unaodhihirika kwa kutokufikiria kuwa tuko bora kuliko watu wengine wakati wote hutusaidia kuhusiana na watu kwa heshima na ukarimu. Katika Mathayo 7:12 Yesu alitupatia maagizo yanayoathiri vile tunavyohusiana na kila mtu tunavyokutana naye mchana kutwa—marafiki, familia, wafanyikazi wenzetu, na hata watu wasiotupenda.

Yesu alisema, “Yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.” Ni wazo rahisi na njia kuu ya kuishi maisha. Ili tushuhudie mambo mazuri kabisa ya Mungu juu ya maisha yetu, tunafaa kutendea watu vile nasi tungependa kutendewa. Tunafaa kutambua mahitaji ya wengine kwanza na kufikiri tunaloweza kufanya ili tuwahudumie.

Maisha yetu yatapungikiwa na mema aliyo nayo Mungu juu ya maisha yetu, iwapo tutamezwa na “nafsi.” Kujifikiria hutukosesha kuona mahitaji ya wengine na kutufanya tukose baraka zinazokuja tunapohudumu. Hatufai kusahau mahitaji yetu kabisa. Lakini tunaweza kufukuza uchoyo wa kibinafsi kwa kutokufikiria kuhusu mahitaji yetu kila wakati.


Iwapo utaanza kuhusiana na watu waliokuzunguka kwa upendo, ukarimu na heshima, utashangazwa vile na itaathiri wanavyohusiana nawe pia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon