Amua Kuendelea

Amua Kuendelea

Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema. —2 WATHESALONIKE 3:13

Lazima sisi sote tukabiliane na kushughulikia masikitiko kwa wakati tofauti. Hakuna mtu aliye hai ambaye kila kitu maishani mwake hufanyika jinsi anavyotaka, kwa njia anayotarajia.

Vitu vinapokosa kunawiri au kufaulu kulingana na mpango wetu, hisia ya kwanza tunayokuwa nayo ni masikitiko. Hii ni kawaida. Hakuna kitu kibaya na kuhisi kusikitika. Lakini tunafaa kujua tutakavyokabiliana na hisia hiyo, au itageuka kuwa kitu kibaya zaidi.

Hatuwezi kuishi ulimwenguni bila kupitia masikitiko, lakini ndani ya Yesu tunaweza kupewa uwezo wa kutokusikitika!

Mtume Paulo alisema kwamba funzo moja muhimu alilokuwa amejifunza maishani lilikuwa kusahau yaliyo nyuma na kuchuchumilia yaliyo mbele! (Wafilipi 3:13-14).

Tunaposikitika, halafu punde kutokusikitika, hivyo ndivyo tunavyofanya haswa. Tunasahau sababu za masikitiko na kuchuchumilia mbele ili kufikilia kile Mungu ametuwekea. Tunapata maono mapya, mpango, wazo, mwono nje mpya, fikra mpya na kubadilisha mtazamo wetu kwa hayo. Kisha tunaamua kuendelea!


Kila siku ni mwanzo mpya kabisa! Tunweza kusahau masikitiko ya jana na kumpa Mungu nafasi ya kutufanyia kitu kizuri leo!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon