Endelea Kufanya Kilicho Sahihi

Endelea Kufanya Kilicho Sahihi

Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema. 2 WATHESALONIKE 3:13

Historia imejaa mifano ya watu ambao ni mashuhuri kwa kufanya vitu vikubwa—ilhali tukichunguza maisha yao, tunapata kwamba walishindwa kabla ya kufanikiwa. Nguvu zao za kweli hazikuwa kipawa chao hata kama ilikuwa nguvu yao. Fikiria kuhusu mifano ifuatayo:

  • Mchezaji wa NBA Michael Jordan aliondolewa kutoka kwa timu ya mpira wa vikapu.
  • Baada ya kusikizwa kwake Fred Astaire alipokea majibu yafuatayo ya uchunguzi: “Hawezi kuigiza. Mwenye upara kidogo. Unaweza kucheza kidogo.”
  • Kitabu cha kwanza cha muuzaji mashuhuri zaidi Max Lucado kilikataliwa na wachapishaji wanne.
  • Walt Disney alifutwa kazi kutoka kw a kampuni ya magazeti kwa sababu alikosa mawazo.

Watu hawa walifanikiwa katika majaribio tofauti tofauti, lakini wote walikuwa na kitu kimoja kilicholingana: uvumilivu. Kukataa kukata tamaa ni mojawapo ya dalili za uhakika, kwa hivyo shukuru kuwa uhakika unaweza kuwa wako ndani ya Kristo. Endelea kufanya kile unaamini ni kitu kizuri kwako wewe kufanya, na hatimaye utafurahia upenyo unaotaka.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba kushindwa kunaweza kuwa kifaa cha kujifunza. Nisaidie leo kuwa na ujasiri na uvumilivu unaohitajika ili kuendelea, hata kupitia kwa kushindwa. Ninakushukuru kwamba, nikiwa nawe katika maisha yangu, nitakuwa nikishinda wakati wote bora tu nisikate tamaa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon