Kwa maana ya haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, mwenye haki ataishi kwa imani. —WARUMI 1:17
Huwa lengo langu kuishi toka imani hata imani. Miaka kadhaa iliyopita, Mungu alinipa ufunuo akaniambia, “Joyce, mara nyingi huwa unatoka imani hata imani, halafu unaenda kwa shaka hadi kwa kutokuamini, kisha unarudi tena kwa imani, na kwenda tena kwa shaka hadi kwa kutokuamini.”
Wakati mwingine huwa tuna mchanganyiko mwingi katika maisha. Wakati mwingine tunakuwa wakakamavu, na wakati mwingine tunakuwa na hofu tele; tuna fikra nzuri wakati mwingine mbaya au tuna imani, lakini tena tuna shaka. Huo mchanganyiko unadhihirika katika mazungumzo yetu, vile tunavyoona katika Yakobo 3:10, “Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu hayafai mambo hayo kuwa hivyo.”
Nina hakika inaonekana vigumu kuwa na imani kila wakati na kutokuwa na shaka, lakini hata kama ni vigumu, kwa Mungu kila kitu kinawezekana. Acha tumwamini Mungu atusaidie kutoka imani hata imani, na kuwa na matumaini ndani yake kila wakati.
Acha kila kitu unachofanya kifanywe na imani, ukizidi kuamini kwamba Mungu yuko nawe na kwamba yu tayari kukusaidia!