Neema ya Kuwa Wajumbe Wake

Neema ya Kuwa Wajumbe Wake

Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. —2 WAKORINTHO 5:20

Wakati mmoja nilipokuwa nikisoma kuhusu mhubiri maarufu na imani yake kuu, nilipendezwa ndani ya moyo wangu na mambo ya ajabu aliyokuwa akifanya katika huduma yake. Nikafikiri, Bwana, ninajua nimeitwa, lakini siwezi kufanya mambo kama hayo. Hapo hapo mara moja, nilihisi Bwana akizungumza na moyo wangu, “Kwa nini?” Si wewe ni una uchafu mwingi tu kama mtu mwingine yeyote?”

Unaona, huwa tunalijua kinyume. Tunafikiria kwamba Mungu anatafuta watu “ambao ni wanyofu.” Lakini huo si ukweli. Neno la Mungu linasema kwamba, Mungu katika neema yake na kibali, huchagua vitu dhaifu na vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima (1 Wakorintho 1:27). Anatafuta watakaojinyenyekeza na kumruhusu kutenda mapenzi yake kupitia ndani yao.

Iwapo utatahadhari ili usije ukawa mwingi wa kiburi, Bwana anaweza kukutumia kwa nguvu kuu kama tu alivyotumia wale wanawake na wanaume wengine wa Mungu. Hatuchagui kwa sababu tunaweza, lakini kwa sababu tu, tunapatikana. Hiyo pia ni sehemu mojawapo ya neema ya Mungu na kibali ambacho huwa anaachilia juu yetu akituchagua kuwa wajumbe binafsi wa Kristo.


Mungu anataka uwe na ndoto katika maisha yako. Na anataka uitimize kwa neema yake unapoendelea kutia imani yako ndani yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon