Heshimu Sauti ya Mungu Juu ya Vyote

Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, ambaye Bwana ni tumaini lake (YEREMIA 17:7)

Mtazamo mmoja unaokaribisha uwepo wa Mungu katika maisha yetu ni mtazamo unaomheshimu juu ya kila mtu na kila kitu. Mitazamo yetu inahitaji kusema, “Mungu, haijalishi anachoniambia mtu yeyote yule, haijalishi ninachofikiria mimi, haijalishi mipango yangu ilivyo, nikikusikia ukisema kitu dhahiri na nijue ni wewe, nitakuheshimu- na kuheshimu unachosema – juu ya vitu vyote.”

Wakati mwingine tunafanya vile watu wanatuambia kuliko vile Mungu anasema. Tukiomba kwa bidii na tusikie kutoka kwa Mungu, halafu tuanze kuuliza watu walio karibu yetu wanavyofikiria, tunaheshimu maoni ya binadamu kuliko ya Mungu. Mtazamo kama huo utazuia uwezekano wetu wa kumsikia Mungu kila mara. Iwapo tutakuwa na uwezo wa kumsikia Mungu na kuongozwa na Roho Mtakatifu kama njia yetu ya maisha, lazima tuache kusikiliza maoni mengi kutoka kwa watu wengi na kuanza kuamini hekima ambayo Mungu huweka ndani ya mioyo yetu. Kuna wakati wa kupokea ushauri mzuri, lakini kuhitaji watu kukubaliana nasi kutazuia mapenzi ya Mungu.

Shetani anataka tufikirie hatuna uwezo wa kusikia kutoka kwa Mungu, lakini Neno la Mungu linasema si ukweli. Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu kwa sababu Mungu anataka tuongozwe na Roho katika njia ya kibinafsi na kujisikilia sauti yake anapotuongoza na kutuelekeza.

Katika andiko la leo, Mungu anasema tutabarikiwa tukimtazama. Kulingana na Yeremia 17:5-6, hulaaniwa anayemtegemea mwanadamu kuwa kinga yake, lakini hubarikiwa anayemtegemea na kumheshimu Bwana. Vitu vizuri hufanyika tukimsikiza Mungu. Anataka kuwa nguvu zetu na lazima tuheshimu Neno lake juu ya vyote.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Sikia kile wengine wanasema, lakini msikilize Mungu.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon