Mfahamu Mungu kama Baba Yako

Mfahamu Mungu kama Baba Yako

Akawaambia, msalipo semeni Baba [yetu uliye mbinguni], jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje… —LUKA 11:2

Kwa muda wa miaka mingi, niliomba “Sala ya Bwana,” na kwa kweli sikumjua Mungu kama Baba yangu. Sikuwa na aina yoyote ya uhusiano wa kibinafsi wa karibu na Mungu. Nilikuwa nikikariri kitu ambacho nilikuwa nimejifunza.

Ukitaka kuwa karibu na Bwana na kuwa na matokeo katika maisha yako ya maombi, ni muhimu kumjua Mungu kama Baba yako. Wanafunzi walipomwambia Yesu awafundishe kuomba, aliwafundisha tunachoita “Sala ya Bwana,” ambayo ni nyumba ya hazina ya kiroho ya kanuni za maombi. Lakini kwanza, Yesu alianza kwa kuwaagiza kusema, “Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.”

Yesu alikuwa anawaonyesha faida ya uhusiano aliokuja kumletea kila aaminiye. Aliwaambia kwamba wangeweza kuwa na uhusiano na Mungu kama Baba yao iwapo walitarajia kwenda kwake kwa maombi. Usiende kwa Mungu kama mtu ambaye unaogopa, lakini anzisha uhusiano wa Baba na mtoto naye. Huo uhusiano wa ndani utakupa uhuru wa kumwomba vitu ambavyo usingemwomba iwapo ungekuwa na uhusiano mkavu wa mbali naye.

Baba yetu wa mbinguni anatupenda na jicho lake liko juu yetu kila wakati.

Jifunze kufurahia Mungu!


Unapoomba, kumbuka una Baba mwenye upendo ambaye anakusikiza.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon