Huna Haja ya Kujitetea

Huna Haja ya Kujitetea

Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano, alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. 1 PETRO 2:23

Tukitaka kufurahia mahusiano ya amani, tutakuwa na hekima kufuata mfano wa Yesu. Alishutumiwa kwa kufanya makosa kila mara, lakini hakujaribu hata mara moja kujitetea. Hakujalishwa na vile watu wengine walivyofikiria juu yake; haikumhangaisha kabisa. Yesu angefanya hivyo kwa kuwa alijua yeye alikuwa nani. Hakuwa na shida na vile alivyojiona. Hakuwa anajaribu kuthibitisha chochote. Alimwamini Baba yake wa mbinguni kuthibitisha kuwa hakuwa na makosa, na, shukuru, tunaweza kufanya vivyo hivyo. Inaongeza amani nyingi kwa maisha yetu tunapogundua kwamba Mungu ndiye mtetezi wetu wa kweli, na tunaweza kuwa watulivu anapokabiliana na mtu yeyote anayetushutumu kwa udanganyifu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninatamani kuishi katika uhusiano wenye afya na amani. Asante kwa mfano wa Yesu ambao unanionyesha kwamba sina haja ya kujitetea. Wewe ni mtetezi wangu, na hilo ndilo ninalohitaji.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon