Je, Una Shauku zaidi ya Mungu?

Maana hushibisha nafsi yenye shauku, na nafsi yenye njaa huijaza mema (ZABURI 107:9)

Tunapokuwa na njaa tunafanya bidii sana kupata chakula. Tunafikiri kuhusu chakula, kuzungumza kukihusu, kwenda madukani kukinunua, na kukitayarisha kwa uangalifu. Ninaamini kwamba tukiwa shauku zaidi ya Mungu katika maisha yetu, tunafaa kufanya vilevile. Mungu alisema kwamba tunafaa kumtafuta kwa mioyo yetu yote, kwa bidii, msisimko, raghba na kwa uzito wote.

Tunatumia muda mwingi kila wiki kwa chakula cha kawaida, lakini tunatumia muda gani kwa chakula cha kiroho? Ninakadiria kwamba wengi wetu wanatumia masaa kumi nan ne kwa wiki wakitafuta, kutayarisha, na kula chakula cha kawaida. Kwa kweli tunafaa kujiuliza muda ambao tunatumia tukimtafuta Mungu na kujifunza kumhusu. Ukaribu wetu kwa Mungu hutegemea muda tunaohiari kutumia katika kukuza uhusiano wetu naye. Wakati ni wa thamani kwetu sisi wote na tunafaa kuutumia kwa vitu ambavyo ni muhimu sana kwetu. Unaweza kuharibu wakati wako au kuwekeza wakati wako; chaguo ni lako. Kile tunachoharibu, huwa tuna poteza , lakini tunachowekeza huturudishia faida.

Ninapendekeza kwamba utumie angalau muda mwingi kumtafuta Mungu jinsi unavyotafuta chakula cha kawaida, na utajazwa kwa hekima na uwepo wake hivi karibuni. Utapata ridhaa ambayo hujawahi kujua kwa kuwa anajijaza katika nafsi yako.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Ni Mungu tu peke yake anayeshibisha nafsi iliyo na njaa, kwa hivyo mpe kipaumbele katika utaratibu wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon