Kuwa na Nia ya Mungu

Kuwa na Nia ya Mungu

Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. —ISAYA 26:3

Yesu alikuwa na ushirika usiokoma na Baba yake wake wa mbinguni kwa sababu alimtazamia Mungu. Inawezekana tu kuwa na ushirika mkamilifu na mtu wakati ambao nia yako iko juu ya huyo mtu. Hili ni funzo tunaloweza kujifunza kama waaminio. Ili kuishi katika ushirika wa karibu na Mungu, ni muhimu kwetu sisi kuishi na “Nia ya Mungu.”

Ni jambo la kuinua mno kuwaza kuhusu wema wa Bwana na mambo yote ya ajabu ambayo ametenda. Ukitaka kuwa na ushindi, chukua muda kila wakati kutafakari juu ya ukuu mkuu wa Mungu. Ukimshukuru Mungu na kuwa na ufahamu wa wema wake ni njia mbili za hakika za kuanza kufurahia maisha.

Yesu alisema kwamba Roho Mtakatifu atatuleta katika ushirika wa karibu naye (Yohana 16:7). Iwapo tutachagua kuwaza kuhusu Bwana, itamleta katika nafasi ya kwanza katika maisha yetu, na tutaanza kufurahia ushirika naye ambao unaleta furaha, amani, na ushindi katika maisha yetu ya kila siku.


Mungu huwa nasi wakati wote, lakini ni muhimu tuwaze kumhusu na tujue uwepo wake uko nasi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon