Maisha ni Safari

Maisha ni Safari

…Na lile wingu lilipoinuliwa walisafiri, au kama lilikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri. HESABU 9:21

Shukuru kuwa furaha yetu maishani haitegemei tu kuwa na hali za kufurahisha. Ni hali ya moyo, uamuzi wa kufurahia kila kitu kwa sababu vitu vyote—hata vidogo, vinavyoonekana kukosa maana—vina sehemu yake katika jumla ya “picha kubwa” ya maisha.

Maisha ni safari. Kila kitu ndani yake ni mchakato. Yana mwanzo, katikati, na mwisho. Sehemu zote za maisha hukua kila wakati. Maisha ni mwendo. Bila kusonga, kuendelea, na kupiga hatua, hakuna maisha. Kwa maneno mengine, mradi tu mimi nawe tuko hai, tutakuwa tunaenda mahali kila wakati.

Iwapo hujakuwa ukifurahia safari ya maisha yako, ni wakati sasa wa kuanza. Iwapo umekuwa ukifurahia maisha yako, basi mshukuru Mungu na utafute njia ya kuyafurahia hata zaidi.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru Baba, kwamba maisha yangu ni safari. Sitakaa nikiwa nimekwama katika hali ngumu au ya majaribu milele —ninaipitia hali hiyo na wewe. Nisaidie kuwa na furaha yako bila kujali mazingira yangu. Nisaidie kufurahia maisha yangu leo!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon