Moyo wa Kunyenyekea

Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, hata sala yake ni chukizo (MITHALI 28:9)

Andiko la leo linasema kitu cha kushangaza kuhusu maombi yetu iwapo hatuna uhusiano unaofaa na mamlaka au tukiwa wakaidi- kwamba ni chukizo kwa Mungu.

Hatuwezi tu kukua au kukomaa bila kurudiwa. Tukiwa wakaidi wa kanuni za kampuni, sheria za trafiki, au mamlaka yoyote yale, basi tuna matatizo makuu ya nia kuliko tunavyoweza kufikiri. Kuwa wakaidi ni kitu tunachopaswa kutia bidii kuondoa katika nia na tabia zetu! Kwa nini? Kwa sababu tukikataa kujisalimisha kwa mamlaka ya kidunia, basi hatutajisalimisha kwa mamlaka ya Mungu. Huo ni ukaidi na utatuzuia kutokana na maombi yenye athari.

Mungu aliniweka katika huduma ya mtu mwingine kwa muda wa miaka kadhaa kabla ya kuniruhusu kuanza yangu. Ilinilazimu kujifunza kuwa chini ya mamlaka. Haikuwa rahisi kwangu. Sikukubaliana na uamuzi uliofanywa kila mara na nikahisi kuwa sikutendewa vizuri, lakini mojawapo ya funzo ambalo Mungu alinifundisha ni kwamba, hatuko tayari kuwa katika mamlaka hadi tujue jinsi ya kukaa chini ya mamlaka.

Unaweza kutaka kupandishwa mshahara au madaraka kazini, ilhali huku unamsengenya au kumkosoa mkubwa wako. Hii ni aina ya ukaidi na inaweza kuzuia maendeleo yako. Kuwa na nia ya kujinyenyekeza na utaona majibu zaidi kwa maombi yako na kusikia sauti ya Mungu kwa uwazi zaidi.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Huenda kila kitu unachoambiwa kufanya maishani kisiwe kizuri, lakini mwishoni Mungu huleta haki.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon