Mungu Anafikiri Wewe ni Wa Ajabu

Mungu Anafikiri Wewe ni Wa Ajabu

Nitashukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu na nafsi yangu yajua sana. ZABURI 139:14 BIBLIA

Huenda usihisi kama wewe unapendeza au ni wa kushangaza, lakini Mungu anasema hivyo juu yako. Zaburi 139 inasema kuwa, “tumeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.” Uchunguzi wa vile mwili wa mwanadamu hufanya kazi unabainisha kwamba kweli sisi ni viumbe wa kushangaza.

Unapompokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako, kitu hufanyika ndani yako. Paulo anaandika kwamba “ya kale (tabia na hali mbaya ya kiroho) yamepita, tazama! Yamekuwa mapya!” (2 Wakorintho 5:17)

Huenda usitambue tofauti yoyote unapotazama kwenye kioo; huenda tabia zako zisibadilike usiku moja; huenda kung’ang’ana kwako kusitoweke ghafla, lakini ukiwa “ndani ya Yesu,” kazi uvumilivu ya mabadiliko huendelea ndani yako polepole. Mungu huona mwisho wa vitu kuanzia mwanzo, na hukuona ukiwa umekamilika ndani yake. Hukuona kupitia kwa Yesu Kristo, kama mtu mpya na mwenye haki kikamilifu.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Nisaidie kujiona vile unavyoniona—mwenye haki, mkamilifu, na anayependwa sana—kupitia kwa Kristo!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon