Kusikiliza, Kupokea, na Kutii Neno la Mungu

Kusikiliza, Kupokea, na Kutii Neno la Mungu

Tazama, nimeyatamani mausia yako, unihuishe kwa haki yako…Nami nitaitii sheria yako daima, naam milele na milele. Nami nitakwenda panapo nafasi, kwa kuwa nimejifunza mausia yako. ZABURI 119:40, 44–45

Furaha yetu hutimilika tunapopokea ahadi za Mungu juu ya maisha yetu na kutii amri zake kwa shukrani. Tunapoamini Neno na kutii chochote ambacho Yesu anatia mioyoni mwetu ili tufanye, tunashinda vitu ambavyo vinajaribu kutufadhaisha au kutuvunja moyo. Kuamini Neno la Mungu hutukomboa kutokana na kung’ang’ana ili tupate utulivu katika ahadi za Bwana. Neno linasema, “Maana sisi tulioamini (kumfuata na kumwamini na kumtegemea Mungu) tunaingia katika raha ile” (Waebrania 4:3). Iwapo fikra zako zimekuwa hasi na umekuwa mwingi wa shaka, huenda ikawa ni kwa sababu umeacha kusikia, kupokea na kutii Neno la Mungu. Mara tu ukianza kuamini Neno la Mungu, furaha yako itarudi na “utakuwa na utulivu” tena. Shukuru kuwa pale mahali pa utulivu ndani ya Mungu ndipo anapotaka uwe kila siku ya maisha yako.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru sana kwa Neno lako. Ninajua kwamba ahadi na mafunzo unayonipa ni kwa faida yangu. Ninaposikia, kupokea na kutii Neno la Mungu leo, nisaidie kuwa na maisha ya furaha timilifu na kushinda ambayo Yesu alikuja kunipa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon