Kuwa Mpiganaji

Kuwa Mpiganaji

Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. —1 TIMOTHEO 6:12

Kama vile tu Mtume Paulo alivyosema kwamba amevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo ameumaliza, imani ameilinda (2 Timotheo 4:7), kwa hivyo alimwaagiza mwanafunzi wake mdogo Timotheo kupiga vita vizuri vya imani. Hiyo ina maana kuwa tunafaa kumwamini Mungu na wakati wote bila kukata tamaa!

Sehemu moja ya kupiga vita vya amani ni kuwa na uwezo wa kutambua adui. Mradi tuko kimya, Shetani atatutesa. Hakuna kitakachobadilika kuhusu hali yetu ikiwa tutakachofanya ni kukaa na kutamani mambo yabadilike. Tunaweza kuchagua kuchukua hatua. Mara nyingi huwa hatumkabili shetani kumpinga anapokuja kinyume nasi na mtamauko au hofu au shaka au hukumu. Huwa tunasikiliza uongo wake, lakini tunafaa kumwambia atokomee!

Mimi na wewe hatufai kuwa mfuko wa ngumi wa shetani; badala yake tunaweza kuwa wapiganaji. Tunaweza kusimama imara katika imani na kujua kwamba Mungu ni mwema na kwamba mambo mazuri yatatufanyikia.

Mungu ni mwaminifu, na tutaona baraka zake zikidhihirika katika maisha yetu tusipokata tamaa. Simama imara! Pigana! Inua ngao yako ya imani! Mungu yuko upande wako na ni vigumu kwako wewe kushindwa ukifmfuata.


Njoo kinyume na Shetani anapojaribu kupata nafasi, na hatawahi kupata ngome.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon