Hata bado ningali na mengi ya kuwaambia lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa (YOHANA 16:12)
Yesu aliwaambia wanafunzi wake maneno ya andiko la leo, kimsingi akiwaambia hawakuwa tayari kusikia kila kitu alichokuwa akitaka kusema, lakini akaahidi kwamba Roho Mtakatifu atakuja kuwaongoza katika ukweli wote (soma Yohana 16:13). Aliahidi kwamba pia Roho Mtakatifu atatufundisha mambo yote na kutukumbusha yale yote ambayo Mungu amesema kupitia kwa Neno lake (soma Yohana 14:26).
Yesu aliposema maneno haya, alikuwa anazungumza na watu ambao alikuwa nao kwa kipindi cha miaka mitatu. Walikuwa naye usiku na mchana, ilhali aligusia kwamba alikuwa na mengi ya kuwafundisha. Tunaweza kufikiria kwamba iwapo Yesu angekuwa nasi binafsi kwa muda wa miaka mitatu, usiku na mchana, tungejifunza mambo yote tuliyohitaji kujifunza. Ninafikiri kwamba ningekuwa na mwezi mmoja na watu bila kukatizwa, ningewaambia kila kitu ninachojua. Lakini Yesu alisema tutarajie mengi zaidi kwa sababu atakuwa na kitu cha kusema kila wakati kuhusu hali mpya tunazokabiliana nazo. Ufunuo wa Mungu na neno lake ni jambo endelezi. Tunapokomaa ndani yake, tunaweza kuelewa kile ambacho tusingeelewa awali. Huenda tukasoma andiko mara kumi halafu wakati ujao tunapolisoma, tunaona kitu ambacho hatukuwa tunajua awali. Unaweza kutarajia Mungu kukufundisha kitu ukisikiliza anachosema na kufunua.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO: Tarajia Roho Mtakatifu kukufundisha kitu kipya kila siku. Fikiria kuandika unachojifunza.