
. . .Nikatazama, nikaondoka, nikawaambia wakuu, na mashehe, na watu wengine waliobaki, msiwaogope; mkumbukeni Bwana, aliye mkuu mwenye kuogofya, mkawapiganie ndugu zenu, na wana wenu, na binti zenu, na wake zenu, na nyumba zenu. Nehemia 4:14
Mstari ulio hapo juu wa (Nehemia 4:14) unatuonyesha Nehemia kama kiongozi wa hekima na nguvu. Hakumtafuta tu Mungu na kumtegemea, alijua kwamba watu hao walihitaji kuwa tayari kupigana katika nguvu za Bwana.
Ningependa kuyapiga mwangwi maneno ya Nehemia kwako leo: Pigania nyumba yako! Pigania watoto wako! Pigania haki yako ya kuishi huru kutokana na hukumu na hatia! Pigania haki yako ya kuishi chini ya neema ya Mungu na usifungike kwa ushikiliaji wa sheria! Pigania haki yako ya kuwa na furaha! Pigania ndoto ambazo Mungu ametia ndani ya moyo wako! Pigania kilicho muhimu kwako! Vile Paulo alivyomwambia Timotheo, tunahitaji kupigana vita vizuri vya imani. Hiyo ina maana kushikilia tu, usikate tamaa, na juu ya yote ufanyayo, amini Mungu kwa sababu Mungu anakupigania na anakusaidia kupigana.
Kataa kuridhika na vitu vichache kuliko vyote ambavyo Mungu anavyo kwa ajili yako, na ushukuru kwamba Mungu akiwa upande wako, hakuna unavyoweza kushindwa vita.
Sala ya Shukrani
Baba, ninashukuru kwamba unanipa nguvu na ujasiri wa kupigania kile kilicho cha muhimu sana katika maisha yangu. Licha ya pingamizi kuonekana kuwa kubwa, ninashukuru kuwa utanipa ushindi kwa Kristo Yesu.