Ujidhibiti sio Kujidekeza

Bali yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai (1 TIMOTHEO 5:6)

Wakati mmoja pete niliyotaka na ningeweza kuinunua kwa sababu nilikuwa nimeweka akiba ya senti fulani. Nilichukua muda kuomba kwa ajili ya jambo hili, nikajaribu hisia zangu kwa kutoinunua mara moja, halafu nikamwuliza Mungu, “Ni sawa kwangu kununua pete hii? Unajua kwamba nitafanya unachotaka nifanye na pesa hizi, lakini ningependa kuinunua iwapo ni sawa.”

Sikuhisi thibitisho lolote kwamba nisiinunue, kwa hivyo nikainunua. Huo ungekuwa mwisho mzuri wa kisa hiki lakini mengine zaidi- bangili. Muuzaji aliniambia, “Iko mnadani hadi kesho. Na inakaa vizuri kwako.” Nilisita lakini nikaenda kumtafuta Dave, nikifikiria, labda ataninunulia.

Dave aliitazama. Alifikiri ilikuwa nzuri na kuniambia, “Ni nzuri kweli, unaweza kuichukua kama unaitaka.”

Nilijua katika moyo wangu sikufaa kununua bangili hiyo. Bila shaka nisingetenda dhambi kwa kuinunua, lakini nilijua manufaa yangu makuu wakati huo yalikuwa kukuza tabia iliyohitajika ya kuacha kitu nilichopenda kweli lakini ambahco sikuhitaji.

Wakati huo nilihisi huenda Mungu angeniachilia kuipata baadaye iwapo nilikuwa bado ninaitaka. Sikuwa na amani ya kuinunua siku hiyo moja niliyonunua pete. Ninapotazama nyuma sasa, ninaona kwamba ujidhibiti niliotumia unaridhisha kuliko ujidekezaji.

Tukiwa tunataka furaha ya kweli, tunahitaji kumsikia Mungu. Atatujulisha iwapo kitu ni sawa kwetu au la.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Acha Mungu akuongoze katika maeneo madogo ya maisha na pia makubwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon