Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana…—YOSHUA 1:8
Neno la Mungu linafunua mawazo yake sahihi yaliyoandikwa kwenye karatasi ili tuyasome na tuyafikirie. Neno linaonyesha vile anavyofikiria kuhusu kila hali na jambo.
Ili kuwa karibu na Mungu, ni muhimu kuruhusu Neno lake kuwa ujumbe unaoishi katika moyo wako. Hili hutimizwa kwa kutafakari kuhusu Neno la Mungu, kuruhusu mawazo yake kuwa mawazo yako. Utakapofanya hivi, utaanza kuwa na mawazo ya Kristo. Ninakuhimiza kupenda Neno la Mungu na uliache liwe nuru inayoongoza maisha yako.
Yoshua 1:8 inatuambia kwamba tunaweza kutenda Neno kiakili ili tupate uzoefu wa kufanikiwa ulimwenguni. Kutafakari au kuwaza Neno la Mungu kuna nguvu za kuathiri kila sehemu ya maisha yetu. Mithali 4:20–22 pia inatuambia kwamba maneno ya Bwana ni chanzo cha afya na uponyaji kwa miili yetu.
Kumbuka kanuni ya kupanda na kuvuna. Kadri ya kiwango cha wakati ambacho mimi na wewe binafsi tunatumia katika kuwaza na kusoma kuhusu Neno la Mungu, ndivyo atakavyotufunulia mawazo yake zaidi.
Mungu huwafunulia mawazo yake walio na bidii ya kusoma Neno.