
Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. WAFILIPI 4:5
Kwa usaidizi wa Bwana, tunaweza kuwa mfano wa ukarimu kwa wale wote tunaotangamana nao. Iwapo wewe ni mpaji badala ya kuwa mchukuaji katika maisha, haitachukua muda mrefu kabla ya watu kutambua kuwa uko tofauti sana na kile walichozoea. Wanaposhuhudia furaha yako, wataona kwamba moyo wenye shukrani na roho ya ukarimu humfanya mtu kuwa mwenye furaha kuliko kuwa mchoyo.
Yesu alituhimiza tuache watu kuona matendo yetu mema na yenye ukarimu ili wakamtambue na kumtukuza Mungu (tazama Mathayo 5:16). Yesu hakumaanisha tuwe wenye kujionyesha au kufanya vitu kwa nia ya kuonekana; alikuwa akituhimiza kutambua vile tunavyowaathiri watu walio karibu nasi. Kwa hakika tunaweza kuwaathiri watu kwa njia hasi, lakini ukarimu huathiri wale walio karibu nasi kwa njia chanya sana, na kutufanya tuwe watu wenye furaha.
Sala ya Shukrani
Baba, ninakushukuru kwa kiwango cha ushawishi ulionipa. Kwa usaidizi wako, nitatumia ushawishi huo kufinyanga moyo mkarimu. Nisaidie, Baba, kuwa nuru gizani leo.