Usaidizi wa Roho Mtakatifu

Usaidizi wa Roho Mtakatifu

Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. —WARUMI 8:5

Warumi 8:5 inatufundisha kuwa tukiyafikiri mambo ya mwili, tutayafuata mambo ya mwili. Lakini tukiyafikiri mambo ya roho tutayafuata mambo ya roho. Matendo yetu huzifuata fikra zetu!

Hebu niseme kwa njia nyingine: Tukifikiri fikra za mwili, fikra mbaya, na fikra hasi, hatuwezi kufuata ya Roho. Inaonekana kwamba fikra zilizogeuzwa, zilizo kama za Mungu ni kitu muhimu cha lazima kwa maisha ya Ukristo yenye mafanikio.

Huenda maisha yako katika hali ya kuvurugika kwa sababu miaka mingi ya kuwaza vibaya. Iwapo ni hivyo, ni muhimu kwako kuelewa ukweli kwamba maisha yako hatayanyoka hadi fikra zako zinyoke. Unafaa kuchukua eneo hili kama mojawapo ya lazima ya muhimu.

Mwombe Mungu akusaidie kujifunza kufikiri mawazo ambayo angetaka uwaze. Huwezi kushinda shida yoyote kwa ukakamavu peke yake. Ni muhimu kuwa mkakamavu lakini mkakamavu ndani ya Roho Mtakatifu, sio katika nguvu za mwili wako. Roho Mtakatifu yuko karibu nawe. Ni msaidizi wako—tafuta usaidizi wake. Mwegemee. Unaweza kufanikiwa kwa usaidizi wake.

Mpe Roho Mtakatifu udhibiti wa maisha yako. Atakuongoza katika mapenzi kamilifu ya Mungu juu yako, ambayo hujumlisha baraka tele, amani na furaha kupita kiasi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon