Woga ni jamaa wa karibu wa majuto. Woga hutuweka kwenye mustakabali, huku majuto yakituweka nyuma. Woga pia una uhusiano wa karibu na hofu. Mara nyingi watu huogopa kufanya kitu kwa hofu ya kitu kinachoweza kufanyika.
Tunajua kwamba Mungu hajatupatia roho wa woga (tazama 2 Timotheo 1:7 Biblia), na kwa kuwa hakutupatia hofu, tunajua kwamba woga hautoki kwake pia. Shukuru kwamba, tunaweza kukataa hisia za woga, huku tukizipiga teke kuondoka katika maisha yetu kabisa.
Acha hii siku iwe siku ya uamuzi kwako—siku ambayo unaamua kutofanya mambo kwa hofu na woga. Kuwa mtu wa sasa hivi. Ishi katika wakati uliopo sio katika wakati uliopita au ujao. Mungu ana mpango juu ya maisha yako sasa. Mwamini leo. Usiahirishe tena.
Sala ya Shukrani
Ninaamini ni mapenzi yako, Baba, kwangu mimi kuishi maisha ya amani na ridhaa. Asante kwamba sihitajiki kutazama nyuma kwa majuto au kutazama mbele kwa woga. Ninachagua kuishi kwenye wakati uliopo ulionipa, huku nikifanya niwezayo katika kila siku mpya.