Usipoteze Mwelekeo

Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona. —MATHAYO 10:39

Maisha huwa na utata wakati mwingine, na ni rahisi kujisahau. Inaonekana kwamba, kila mtu hutarajia kitu tofauti kutoka kwetu. Kuna shinikizo linalokuja kwetu kutoka kila upande la kuwapendeza watu wengine na kutimiza mahitaji yao.

Tukijaribu kuwa kile wengine wanataka tuwe, katika mchakato huo, huenda tukajisahau. Huenda tukakosa kutambua kusudi la Mungu juu yetu kwa sababu tunajaribu kwa nguvu kupendeza kila mtu ilhali sisi wenyewe hatupendezwi na tulivyo.

Kwa miaka mingi, nilijaribu kuwa vitu vingi ambavyo sikuwa, na nikachanganyikiwa kabisa. Ilibidi niondoke kwenye huo mzunguko na kujiuliza: “Ninaishi kwa ajili ya nani? Ninafanya haya yote kwa nini? Kwani nimekuwa tu mtu wa kupendeza watu? Je, niko ndani ya mapenzi ya Mungu juu ya maisha yangu?”

Je, umejisahau pia? Umefadhaika kutokana na kujaribu kutimiza mahitaji ya watu wengine huku ukihisi kutokutimizika? Ikiwa ndiyo, unaweza kuchagua kuchukua msimamo na uamue kujitambua, kutambua mwelekeo wako na mwito wa Mungu—mapenzi ya Mungu juu ya maisha yako. Utajitambua kwa kumkaribia Mungu, kutambua mapenzi yake juu ya maisha yako, na kuyafanya.


Ukiutwaa moyo wako kutenda mapenzi ya Mungu, utatambua nafsi yako ya kweli.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon