Usiwahi Kusalimu Amri

Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho (WAGALATIA 6:9) 

Sababu moja ya watu kutosikia sauti ya Mungu ni kwamba wanasalimu amri mapema sana. Paulo na Sila walipatikana wakiwa bado wanaabudu na kumsifu Mungu kizuizini usiku wa manane (soma Matendo ya Mitume 16:25). Watu wengi wangesalimu amri na kwenda kulala mapema. Wito wetu unafaa kuwa: “Usisalimu amri.” Ninakuhimiza usisalimu amri katika kuzungumza na Mungu na kumngoja azungumze nawe, hata ikawaje. Tumia muda na Mungu kila wakati. Mtu anayekataa kusalimu amri ni yule ambaye Shetani hawezi kushinda. Anataka usalimu amri sasa hivi na kusema vitu kama:

  • “Sitawahi kupata kazi.”
  • “Sitawahi kuolewa.”
  • “Sitawahi kutoka kwa madeni.”
  • “Sitawahi kupunguza uzani.”

Nia kama hizi zinaweza kuhakikisha hatupati chochote! Lakini tunaweza pia kuchagua nia inayosema, “Mungu ni mwaminifu kwa Neno lake na sitawahi kusalimu amri.” Mojawapo ya sababu kubwa hufanya watu wasione matokeo ya maombi yao ni kwamba huwa wanasalimu amri. Tutavuna hivi karibuni, lakini ni lini? Ni wakati ambao Mungu anajua tuko tayari kupokea kile tunachoomba. Hadi wakati huo utimie, kazi yetu ni kusalia tukiwa waaminifu. Endelea kuomba na uendelee kutii.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu hutupatia nafasi ya pili, kwa hivyo iwapo unahitaji mwanzo mpya, leo ndiyo siku!  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon