Wekeza katika Uponyaji Wako

Wekeza katika Uponyaji Wako

Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. WAEBRANIA 10:36

Baraka ilioje kujua kuwa Roho Mtakatifu hutusaidia kushinda mambo yetu ya kale. Shukuru kuwa kwa imani na subira, unaweza kupona kutokana na uchungu wako wa kale, kutokana na vitu ambavyo umefanyiwa, au kutokana na makosa uliyofanya, lakini uponyaji huo utahitaji uwekezaji wa wakati kutoka kwako. Unaweza kuanza kuwekeza katika mashaka yako au unaweza kuanza kuwekeza katika uponyaji wako.

Njia mojawapo ambayo unaweza kukabiliana na mambo yako ya kale, ni kwa kukiri ahadi za Mungu badala ya kuongea kuhusu hisia hasi za kushindwa. Unapokiri ahadi za Mungu badala ya shida zako, unafanya mazoezi ya imani yako na kuwekeza katika uponyaji wako. Hii ni njia ya nguvu ya kuanza kufurahia maisha yako.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba ninaweza kuwekeza katika uponyaji wangu kwa kukiri Neno lako juu ya maisha yangu. Nisaidie kuona ahadi zako badala ya shida zangu. Asante kwa kuwa umenihifadhia vitu vizuri kwa ajili ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon