Roho Mtakatifu ni Mwungwana

Ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani (WAGALATIA 3:14)

Katika kitabu hiki, nimeandika mengi kuhusu Roho Mtakatifu na kuhusu kujazwa na Roho, na ninataka kuhakikisha una nafasi ya kujua Roho Mtakatifu kwa njia hii unaposafiri katika kurasa hizi.

Roho Mtakatifu ni mwungwana. Hawezi kujilazimisha katika maisha yako katika ukamilisho wake bila kualikwa. Atakujaza lakini ukimwomba tu kufanya hivyo. Katika Luka 11:13, Yesu anaahidi kwamba Mungu atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwitisha. Na Yakobo 4:2 inatuambia kwamba sababu ya kukosa vitu fulani ni kwamba hatuombi vitu hivyo.

Ninakuhimiza kwenda kwa ujasiri mbele za Mungu na kumwomba kukujaza kwa Roho Mtakatifu kila siku. Omba ukitarajia kupokea. Usiwe mwenye nia mbili au au kuruhusu shaka kujaza moyo wako, lakini omba kwa imani. Amini kwamba umepokea, na ushukuru Mungu kwamba anaishi ndani yako. Mungu si mtu, aseme uongo (soma Hesabu 23:19). Ni mwaminifu kwa kutimiza Neno lake wakati wowote mtu anapochukua hatua ya imani, kwa hivyo omba na upokee, kwa hivyo ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu (soma Yohana 16:24).

Andiko la leo linasema, kwamba tunapokea ahadi ya Roho kwa imani. Karama haziwezi kulazimishwa mtu; lazima zipewe na mtoaji halafu zipokewe na wale wanaopewa. Mungu hutoa Roho wake kwa hivyo unachohitaji ni kutulia na kupokea kwa imani.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usiwahi kuona haya kuomba na kuendelea kuomba Mungu kukutana na mahitaji yako yote.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon