Ninafaa Kuomba Mara Ngapi?

Ninafaa Kuomba Mara Ngapi?

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa, kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. —MATHAYO 7:7– 8

Siamini kwamba tunaweza kuweka kanuni kwa suala kuhusu ni mara ngapi tunaweza kuomba kuhusu kitu kilekile. Lakini ninafikiri kwamba kuna miongozo ambayo inaweza kutumiwa kutusaidia kuwa na hakikisho katika nguvu ya maombi.

Watoto wangu wakihitaji kitu, huwa ninataka waniamini kufanya walichoniambia niwafanyie. Sitajali, na ninaweza hata kupenda iwapo mara moja moja wataniuliza, “Mama, ninangoja kupata hivyo viatu vipya.” Hiyo taarifa itanitangazia kuwa wanaamini nitafanya nilichoahidi. Watakuwa wananikumbusha ahadi yangu lakini sio kwa njia ambayo itatia doa uadilifu wangu. Ninaamini kwamba wakati mwingine tukirudiarudia kumwomba Mungu kitu kilekile, ni ishara ya shaka na kutoamini, sio ya imani na uvumilivu.

Nikimwitisha Mungu kitu katika maombi na ombi hilo lije mawazoni mwangu baadaye, nitazungumza naye kulihusu tena. Lakini nikifanya hivyo, nitajiepusha kumwomba kitu hichohicho kama ambaye ninafikiri hakunisikia wakati wa kwanza. Ninamshukuru Bwana kwamba anaishughulikia hali niliyokuwa nimeombea awali na kutarajia kwamba atatenda yaliyo mema.


Maombi ya imani bila kikomo hujenga imani na hakikisho ndani yetu tunapoendelea kuomba.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon