Upendo wa Mungu Hushinda na Hubadilisha

Upendo wa Mungu Hushinda na Hubadilisha

Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. —LUKA 15:20

Mtu yeyote anaweza kubadilishwa kabisa na kwa dozi za mara kwa mara zisizokoma za upendo wa Mungu. Haijalishi walichofanya maishani au vile huenda tukawafikiria kuwa wazuri au wabaya, Upendo wa Mungu unaweza kuutia vuguvugu hata moyo ulio baridi kabisa.

Dini mara nyingi huwapa watu kanuni za kufuata na sheria za kutii. Huwafanya waamini lazima wachume kibali na upendo wa Mungu kupitia kwa kazi nzuri. Hicho ni kinyume kabsia cha mafunzo ya ukweli wa kibiblia.

Neno la Mungu linasema kwamba huruma hujitukuza juu ya hukumu (Yakobo 2:13). Ni wema wa Mungu unaovuta watu wapate kutubu (Warumi 2:13), siyo kutii sheria kanuni. Yesu alikuja kutupatia kitu kilicho bora kuliko dini—Alikuja kutupatia uhusiano wa kibinafsi wa upendo na wa karibu na Baba kupitia kwake.

Upendo wa Mungu usio na masharti hauruhusu watu kubaki vile walivyo; badala yake, unawapenda huku wakiendelea kubadilika. Yesu alisema kwamba hakuja kwa ajili ya wenye afya, bali kwa waliougua (Mathayo 9:12). Ulimwengu wetu mwingi leo unaagua, na hakuna jibu kwa kinachouuguza, isipokuwa Yesu Kristo na yote anayowakilisha.


Upendo usio na masharti utashinda uovu na kubadilisha maisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon