Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu. 1 PETRO 1:3
Rehema za Mungu kwetu sisi ni kitu cha kutusababisha kushukuru wakati wote. Wakati mmoja Charles Spurgeon alisema, “Rehema za Mungu ni kuu kiasi cha kwamba unaweza kukausha maji yote baharini au kulinyima jua mwangaza wake au kufanya anga liwe finyu sana, lakini huwezi kupunguza rehema kuu za Mungu.”
Waah! Fikiri kuhusu hilo. Kuna mmoja wetu anayeweza kukausha maji baharini? Tunaweza kukausha maji kwenye bakuli la kuoga au bwawani…lakini sio baharini! Hilo linakupa wazo la rehema kubwa aliyo nayo Mungu juu yetu.
Ingawa Mungu anachukia dhambi, na dhuluma humkasirisha, si Mungu wa hasira! Amejaa rehema, hatuhesabii makosa yetu. Hatuwezi kufanya makosa mengi sana kiasi cha kukosa rehema juu yetu. Shukuru kwamba mahali palipojaa dhambi, neema hujaa zaidi pia.
Sala ya Shukrani
Baba, ninashukuru kwa rehema zako katika maisha yangu. Hata kama hujafurahishwa na dhambi zangu, ninajua kwamba unanipenda na unasikia maombi yangu. Asante kwamba unasamehe dhambi zangu na kuwa tayari kunisaidia kuanza tena.